Wakazi wa kikjiji cha Njisi Wilayani Kyela kupitia Mheshimiwa diwani Ndugu Omari R. mwinjumali wameweza kutoa eneo kubwa la kujenga shule ya Sekondari baada ya kutambua tatizo kubwa linalowakabili watoto wa shule wanaomaliza darasa la saba katika kijiji chao akizunguza mbele ya Afisa habari wa Halmashauri Ndugu Fredy Kabutu, Mh diwani alisema ni kwa miaka mingi sasa kijiji hicho kimekosa shule ya sekondari huku idadi ya wanafunzi wanaomaliza kikjijini hapo ikizidi kuongezeka. Hata hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Kyela iliweza kutuma watalamu wa ardhi na kwenda kulipima eneo hilo na kuridhishwa na jitihada kubwa walizozifanya viongozi wa kijiji hicho pamoja na wananchi na kuahidi kuanza kuchukua hatua za haraka kuanzisha mradi huo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa