Kauli hiyo imezungumzwa na mkuu wa wilaya ya Kyela mhe. Claudia Kitta katika mkutano wa baraza la madiwanai, lililofanyika siku ya jumanne tarehe 27/08/2019, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kyela.
Mkuu wa wilaya ameagiza watendaji na wananchi wote kushirikiana kwa pamoja ili kufichua wahalifu wanaosababisha mauaji kwa raia katika wilaya ya Kyela, jambo hili linatishia amani kwa raia kwani mpaka sasa vifo vya watu watano vimeripotiwa kutoka vijiji vya Njisi, Nkuyu na Ipinda.
Aidha alisema vijiji vyote vinatakiwa kupambana na wahalifu kwa nguvu zote ili kukomesha vitendo hivyo vya kikatili mara moja. Pia mwenyekiti wa baraza la madiwani Dr.Hunter Mwakifuna amewataka madiwani kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, katika zoezi zima la kuwasaka wahalifu ili kuwachukulia hatua za kisheria mara moja.
Aidha kwa vyombo vya ulinzi na usalama, kwa kushirikiana na viongozi wa wilaya wameombwa kupambana kwa nguvu zote kuwatafuta wahalifu ili kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya kisheria.
Baraza la madiwani limefanyika ili kujadili na kutoa tathimini ya mafanikio yaliyojitokeza katika mwaka wa bajeti 2018/2019. Pia baraza hilo limejipanga kushughulikia changamoto zote zinazojitokeza katika kuleta maendeleo ndani ya wilaya ya Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa