Katika hatua ya kuhakikisha usalama wa afya za wananchi na kudhibiti biashara haramu mipakani, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Bw. Audas Temba ameongoza zoezi la uteketezaji wa bidhaa mbalimbali haramu zilizokamatwa zikiingizwa nchini kutoka nchi jirani ya Malawi kwa njia ya magendo. Bidhaa hizo ni pamoja na nguo za ndani za mitumba, pombe kali zenye kiwango kikubwa cha alcohol, na bidhaa nyingine zilizokwisha muda wake wa matumizi (expire), ambazo kwa mujibu wa mamlaka, ni hatari kwa afya ya binadamu.
Zoezi hilo lilifanyika leo tarehe 30.06.2025 Kata ya Ngana katika eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kuteketeza bidhaa hizo na kuhudhuriwa na Maafisa wa forodha ya mpaka wa Malawi na Tanzania, Wataalam kutoka Ofisi ya Mkurugenzi, Kamati ya ulinzi na usalama, .
Bw. Kessy Temba alitoa wito kwa wananchi wa Kyela na maeneo ya mpakani kuwa walinzi wa kwanza wa usalama wa afya zao na uchumi wa taifa kwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi wanapobaini harakati za biashara za magendo.
Akizungumza katika tukio hilo, Afisa Forodha wa mpakani mwa Malawi, Bw. Alex Getau alisema kuwa moja ya sababu kuu za kuteketeza bidhaa hizo ni kuzuia madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kwa wananchi endapo bidhaa hizo zingeingia sokoni. Alisema baadhi ya bidhaa zenye madhara makubwa kama pombe kali zenye viwango vya juu vya alcohol, vinaweza kusababisha athari za kiafya ikiwemo matatizo ya ini, figo na hata vifo vya ghafla kwa watumiaji.
Bw. Getau aliongeza kuwa hatua hiyo pia inalenga kukomesha tabia ya wafanyabiashara wachache wasiowaaminifu wanaoingiza bidhaa nchini kwa njia za panya, hali inayosababisha kuharibu soko la bidhaa halali zinazouzwa na wafanyabiashara waaminifu.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa