IDARA YA AFYA
Majukumu ya Idara ya Afya ni kama ifuatavyo:-
ENEO
|
HALI ILIVYO
|
CHANGAMOTO
|
Idadi ya Vituo Vya kutolea Huduma
|
Halmashauri ina Vituo 50 vya kutolea huduma za Afya, kati ya hivyo Hospitali 3, Kituo cha Afya 1, kliniki (2). Kati ya vituo hivi, 30 vinamilikiwa na serikali, 3 vya mashirika ya dini, 10 vya watu binafsi na 1 shirika la umma (Kiwira Coal Mine).
|
Vituo vya kutolea huduma bado havina watoa huduma wa kutosha kuna baadhi ya vituo wapo (2) na vituo vya kutolea huduma havitoshi katika wilaya.
|
Watumishi
|
Idara ya Afya unauhitaji wa watumishi 579 kwa mujibu wa ikama,na kwa sasa watumishi waliopo ni 371 sawa na asilimia 64%.na ina upungufu ya watumishi 208 sawa asilimia 36% huo unazihusu kada zote za watumishi na kwa watumishi wenye ujuzi unaohitajika (Skilled staff).
|
Tunachangamoto kubwa na upungufu watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya.
|
Huduma za Wazee zaid miaka 60 ,wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.
|
Hadi kufikia 19,725 jumla ya wazee wametambuliwa na wanaendelea kupatiwa huduma katika vituo vyote vya kutolea huduma kwa kutumia vitambulisho vyao bila usumbufu wa aina yeyote.
|
Kundi la wanaotibiwa kwa misamaha kuwa kubwa sana hivyo fedha inayochangiwa ndio inayotumika kuhudumia makundi maalum.
|
Mfuko wa Afya ya Jamii Ulioboreshwa(Ichf)
|
Halmasuri ya wilaya ina Jumla ya kaya 54,000 katika halmashuri 1033 zilizojiunga na ichf ni sawa na 1.9%
|
Changamoto wananchi hawajiungi na Ichf iliyoboreshwa lakini uhamasishaji wa kujiinga unaendelea
|
Miradi ya Ujenzi
|
Miradi inayoendelea katika idara ya afya, ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, na zahanati sita (6) zipo kwenye hatua maboma Kapamisya, kyangala, mwambusye, kasala, Isaki na kasumulu
|
Uhaba wa fedha za kumalizia maboma,uchakavu na ufinyu wa majengo katika hospitali ya wilaya.
|
Miradi ya Ujenzi
|
Miradi inayoendelea katika idara ya afya, ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, na zahanati sita (6) zipo kwenye hatua maboma Kapamisya, kyangala, mwambusye, kasala, Isaki na kasumulu
|
Uhaba wa fedha za kumalizia maboma,uchakavu na ufinyu wa majengo katika hospitali ya wilaya.
|
Hali ya Dawa
|
Upatikanaji wa dawa kwa robo ya tatu ni asilimia 97.5%
|
Kwa mwaka wa fedha 2020 /21Idara ilitegemea kupata fedha kiasi cha Tsh. 455,689,891/=kwa ajili ya dawa na vifaa tiba toka serikali kuu lakini fedha hiyo hazijapokelewa mpaka sasa, hivyo ku hivyo kuathiri hali upatikanaji wa dawa katika vituo.
|
Makusanyo ya fedha za uchangiaji wa huduma katika zahanati na kituo cha afya.
|
Zahanati fedha ya uchangiaji ni shilingi 3000/= kituo cha afya ni shilingi 5000/=
|
Fedha hii ya uchangiaji ni ndogo hivyo kuathiri uendeshaji wa huduma vituoni.
Makusanyo kwa wiki kwa zahanati ni kiasi kisichozidi 50,000/= misamaha 2,000,000/= na kituo cha afya makusanyo kwa wiki ni 400,000/= na misamaha 1,100,000/=. hospitali makusanyo kwa wiki ni 7,000,000/=,misamaha 4,000,000/= |
Bomani Street
Postal Address: P. O box 320 Kyela
Telephone: 025-2540035/7
Mobile: 0756944794
Email: ded@kyeladc.go.tz
Copyright ©2017 Kyela District Council . All rights reserved.