Wanafunzi wa shule ya Msingi Shiboya iliyopo wilayani Rungwe, imetembelea katika banda la Kyela Nanenane lililopo katika viwanja vya Mwakangale Mbeya leo asubuhi, tarehe 06/07/2019.
Akiongea kwa niaba ya Wanafunzi mwalimu Happiness Nombo ambae ni mwalimu wa michezo amesema, wamevutiwa kutembelea banda la Kyela kwa kuwa na vitu vingi vya kuvutia.
Aidha amesema amependa wataalam kutoka Kyela walivyowapokea Wanafunzi wao na kuwapa elimu juu ya uwepo wa vivutio vya utalii,magonjwa ya macho, kilimo cha bustani na mambo mengine mengi.
Banda la Kyela (Nanenane) limekuwa likitembelewa na wananchi wengi sana tangu lilipofunguliwa siku ya tarehe 01/08/2019. Na kikubwa kinachowavutia watu ni uwepo wa vitu vingi vya asili kama vyombo vya udongo wa asili, dagaa wa ziwa Nyasa, uwepo wa wajasiliamali ambao wanatoa huduma za elimu za ubunifu kwa wananchi.
Pia uwepo wa Madaktari wa macho, Maafisa kilimo wanaotoa elimu juu ya kilimo bora imekuwa ni chachu kwa wananchi kuzidi kufurika katika banda hili.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Ofisi Ya Habari Na Mawasiliano
Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa