Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Bi.Florah A Luhala ameongoza kikao cha tathmini ya hali ya usafi wa mazingira kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 10.4.2025.
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji Bi.Florah A. Luhala amewataka Watendaji kutekeleza yaliyomo kwenye mkataba wa tarehe 14.8.2024 ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.
Mkurugenzi huyo amewaagiza wataalamu wa afya pamoja na Watendaji kata kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya usafi wa Mazingira ikiwemo matumizi sahihi ya vyoo ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
Aidha Mkurugenzi amewaasa Watendaji kusimamia utunzaji wa vyanzo vya maji vinavyopatikana kwenye maeneo yao ili kuhakikisha Wananchi wanapata maji safi na salama.
Bi.Florah Luhala amewataka Watendaji kuwa na utaratibu wa kuwasilisha taarifa za usafi wa mazingira kwa wakati ili kubaini changamoto zilizopo katika kata zao.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa