Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Halima Mdee imefanya ziara ya kukagua Miradi ya maendeleo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyela ambayo ni mradi wa Shule ya Sekondari ya wasichana Mbeya Girls, pamoja na jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela tarehe 20.03.2025.
Akikagua miradi hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mhe.Halima Mdee amemtaka Mkurugenzi Mtendaji aendelee kusimamia vizuri fedha zinazoletwa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili iweze kunufaisha kila Mwananchi.
Mhe. Mdee ameitaka Ofisi ya Mkurugenzi kusimamia Miradi ya maendeleo kwa weredi mkubwa ili kuifanya Miradi hiyo iwe na ubora zaidi.
Naye, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe.Dkt Festo Dugange ameiagiza ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kufuata maelekezo yote waliyopewa na kamati hiyo juu ya miradi iliyokaguliwa.
Sambamba na hilo Mhe. Dkt Dugange amelitaka Baraza la Madiwani kuimarisha ushirikiano uliyopo na Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi ili kuhakikisha Fedha za Miradi ya maendeleo zinatumika ipasavyo na Miradi inakamilika kwa Wakati uliokusudiwa.
Aidha Kamati hiyo ya Bunge imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuzingatia ubora katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela ukiwemo mradi wa jengo la mama na mtoto.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Josphine Manase amesema maelekezo yote ya kamati yatafanyiwa kazi na kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali ya awamu ya sita kwa ajili ya utekelezaji wa miradi zinatumika ipasavyo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa