Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Ndg.Gerlad Mlelwa amehitimisha mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Manunuzi NeST kwa Walimu wakuu,walimu wa manunuzi,wakuu wa Shule ,watendaji wa Kata na wa vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela katika Ukumbi wa Sisita Hall tarehe 24.4.2025.
Akihitimisha Mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi amewapongeza washiriki hao kuwa miongoni mwa wanufaika wa Mafunzo hayo na kuwataka kutumia mafunzo hayo kama fursa ya kujua hatua zote zinazohitajika kwenye mfumo huo.
Ndg.Gerlad Mlelwa amesema hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaokwenda kinyume na kanuni za mfumo wa NeST kama walivyoelekezwa na Kufanya Manunuzi nje ya Mfumo wa Nest ni Kinyume cha Sheria
Aidha Kaimu Mkurugenzi amefafanua kuwa, "Mfumo huu wa kielektroniki umeundwa ili kuboresha uwazi, ushindani, na usawa katika michakato ya manunuzi ya umma, hivyo tunaamini kwa mafunzo haya yatasaidia kutatua changamoto hususani kuharakisha michakato ya manunuzi ya vifaa vya ujenzi na upatikanaji wa mafundi kwani mfumo ni rafiki na kufanikisha Miradi ya Maendeleo kumalizika kwa wakati
Kwa upande wake Ndg. Anthony Masau Afisa kutoka mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) Nyanda za juu kusini anaamini kwamba mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo walimu wakuu,walimu wa manunuzi, wakuu wa shule,watendaji wa kata na wa vijiji yanalenga kuwawezesha kutumia mfumo wa NeST kwa ufanisi bila vikwazo na panapotokea changamoto PPRA ipo tayari muda wote kutoa usaidizi"
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa