Mhe; Josephine Manase Mkuu wa wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya,amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha mapinduzi (CCM) katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri tarehe 29/03/2025, kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2024 kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Mhe:Manase katika taarifa yake amesema Sekta ya Fedha imeongeza uwazi na matumizi kwa utoaji huduma kwa kutumia TEHAMA,Halmashauri imetoa Mafunzo ya Mfumo wa Mapato na Matumizi katika Vituo vya kutolea huduma (FFARS) kwa Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji Pamoja na kuwasajili.
Pia Mkuu wa Wilaya aliwaeleza wajumbe wa kamati ya Siasa Wilaya ya Kyela kuwa katika kipindi cha kuanzia Mwezi wa Julai 2024 hadi Desemba 2024,Halmashauri imekusanya jumla ya Shilingi Billion 4.7 (4,791,965,052.04) sawa na asilimia 83.81 ya Makisio ya bajeti ya Shilingi Billion 5.7 (5,717,763,000.00).
Aidha Idara ya Mipango na Uratibu inaendelea na majukumu yake ya Msingi ya kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambapo Halmashauri kwa Mwa
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa