Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu Ezekiel H. Mgehema (kulia).
Haya yamezungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu, Ezekiel H. Magehema alipokuwa katika ziara ya kutembelea ujenzi wa jengo la upanuzi wa zahanati ya Kilasilo iliyopo katika kata ya Ikimba hapa wilayani Kyela.
Mkurugenzi amefanya ziara hiyo leo tarehe 14/07/2020, akiwa na wakuu wa Idara na vitengo, lengo la ziara ni kuwapa uhuru wakuu wa Idara na vitengo kulikagua jengo hilo, na kuangalia baadhi ya mapungufu, ili waweze kujadiliana jinsi ya kuyarekebisha kabla ya kuja kukaguliwa na viongozi kutoka ngazi za juu.
Aidha Mkurugenzi alitoa shukrani zake za dhati kwa wananchi ambao waliwasilishwa na mwenyekiti wa kamati ya ujenzi, ndugu Asajile Jonstoni akiwa na Afisa Mtendaji wa kata hiyo. Alisema, niwapongeza wananchi wa kata hii kwa kujitolea kusaidia kazi mbalimbali katika ujenzi wa jengo hili, ila kama serikali imetoa milioni 200,000,000/=, tulitegemea kuwa na majengo mengi zaidi, hivyo wakati mwingine nguvu za wananchi ziongezeke ili kupata majengo mengi zaidi, pale tunapopata pesa za msaada kama hizi kutoka serikali kuu.
Nae Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu, Mariam Ngwere, alitoa ushauri kwamba, ni vizuri jengo hili likaendelea kutoa huduma ndogo ndogo, pale marekebisho madogo madogo yanapoendelea kufanyika.
Mwisho Mkurugenzi Mtendaji aliwataka wataalam kutoka ardhi, kuhakikisha eneo lote la zahanati, kuwa na mipaka inayofahamika ili kuondoa, migogoro ya mipaka baina ya Halmashauri na wanakijiji.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa