Tarehe 12Februari 2008,Mh Rais J.M.Kikwete alitoa tamko la kugatua usimamizi na uendeshaji wa shule za sekondari.
Kwa kuzingatia sera na sheria za elimu ,Majukumu ya Idara hii ni kama ifuatavyo
Kuhakikisha kuwepo kwa mazingira mazuri ya kujifunza na kufundisha
Kusimamia kikamilifu uandikishaji wa wanafunzi wote wenye sifa ya kujiunga na elimu bila kujali jinsia,Ulemavu n.k na kuhakikisha kuwa wote walioandikisha wanamaliza masomo
Kusimamia taaluma ya Walimu na Wanafunzi wote
Kuendesha na kusimamia kikamilifu mitihani yote ya ndani na kitaifa katika ngazi ya Wilaya
Kuibua na kusimamia vipaji mbalimbali vya wanafunzi kupitia mashindano kama vile UMISSETA
Kusimia utendaji wa kazi za walimu kwa kuzingatia sheria kanuni na miongozo mbalimbali na kuhakikisha maslahi yao yanapatikana kwa wakati(Wajibu na haki za watumishi)
Kuwa kiungo muhimu kati ya Jamii na Mamlaka ya serikali za mitaa katika mambo yanahusu elimu ya sekondari.
Kufanya tathmini za mitaala kwa kutumia nyenzo ikiwemo mitihani mbalimbali ya kitaifa na ndani.
Kutunza na kuboresha takwimu sahihi za elimu na miundombinu yote ya shule za sekondari.