Thursday 21st, November 2024
@Kyela
YALIYOJILI KATIKA ZIARA YA MHE. WAZIRI WA KILIMO JAPHET HASUNGA AKIWA KYELA
Nimefurahi kusikia kuwa Kyela;
1.Hakuna upungufu wa chakula
Lakini hii ni kwasababu ya wakulima.
2.Mtu yeyote akibeze kilimo huyo tutampima akili.
3.Kunipongeza kwenu kutakuwa na maana Sana kama nitatekeleza majukumu yangu vizuri.
4.Kwetu Mbozi hatujawahi kupata waziri, namshukuru Mhe. Rais kunichagua na kuifungua Mbozi
5.Wilaya ya Kyela inaaminika kwa msimamo
6.Kokoa bora Duniani inatoka Kyela
7.Kokoa ni almasi pia ni dhahabu itunzeni
8.Nitashangaa Mkurugenzi kama wewe ushindwe na Chunya kwa kilimo cha Korosho
9.Nitasimamia kuhakikisha zao la korosho mnada wake kuanza kufanyika Kyela
10.Fufueni zao lenu la Mpunga Kyela kwa mbegu za asili
11.Sitawasahau kuwaletea miche ya
Michikichi
12.Anzisheni kilimo cha mboga na matunda kwa maana Serikali ipo kwenye mpango wa kununua ndege ya mizigo itakayokuwa ikitua Songwe, kwa ajiri ya kubeba mbogamboga na matunda kupeleka nje ya nchi, tuitumie fulsa hii.
13.Kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi akipinga ushirika nitamshangaa Sana maana hiyo ndio Ilani ya Chama inavyotaka tuitekeleze.
14.Kyela ni maarufu kwa kufurahia kuona watu wanagombana, hilo ni pepo likemewe.
15.Wezi wote lazima wachukuliwe hatua
16.Ushirika hauta kufa na mazao ya korosho yataendelea kuuzwa kwa ushirika.
17.Naenda kushughulikia upatikanaji wa magunia ya Korosho
18.Maeneo yenu yanafaa kulima mara 2 Kwa mwaka
*maagizo*
1.Nimemwagiza mkurugenzi katika bajeti hii atenge pesa kwa ajili ya kuanzisha skimu kubwa 2 za umwagiliaji
2.Kila mkulima afungue akaunti yake
3.Ghala kuu lilifungwa lifunguliwe ndani ya mwezi mmoja
4.Mawakala walete pembejeo za kutosha kwani huu ndio msimu wa kilimo.
5.Mkuu wa Wilaya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama simamieni minada ya Kokoa.
6.Takukuru kamata wezi wote waliokula pesa ya mkulima.
7.Mkuu wa Wilaya kamata NJEMKE kamata wote kwanzia sasa.
8.Kila mkulima wa kokoa atambulike na kuwe na daftari la kudumu.
9.Chuo cha Uyole wafanye utafiti wa mbegu zetu za asili ili zianze kutumika mara moja.
10.Tununue mbolea zinazoendana na udongo halisi
11.Maafisa ushirika kutoka tume, nimeambiwa kuna AMKOS 18, NATAKA zikaguliwe zote ndani ya mwezi mmoja.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa