Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Josephine K. Manase amehitimisha mafunzo ya uongezaji wa thamani mazao ya kilimo kwa wanawake wajasiriamali wilayani Kyela.
Akihitimisha mafunzo hayo ya siku 3 katika ukumbi wa Chuo cha "KPC" leo tarehe 6/05/2023, Mheshimiwa Manase amesema;
Anatoa shukrani zake za dhati kwa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kwa kutoa mafunzo kwa wanawake 55, ambapo anaamini mafunzo hayo ya uongezaji wa thamani kwa mazao ya kilimo yataleta matokeo chanya katika wilaya yetu ya Kyela na Taifa kwa ujumla.
Aidha Mhe. Mkuu wa wilaya, ametoa shukrani zake za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga mazingira mazuri ya ufanyaji wa biashara nchini, ikiwa ni pamoja na kufungua fulsa kwa wanawake wajasiriamali.
Amesema Mhe. Rais amefanya mapinduzi makubwa katika sekta za Utalii, Kilimo Afya, Elimu, Mahusiano kimataifa, miundombinu ya usafirishaji, mfano mzuri ni uwepo wa meli zetu kubwa 2 za mizigo na 1 ya abiria katika ziwa Nyasa, Ujenzi wa barabara kutoka Ibanda hadi bandarini Kiwila na Itunge hapa wilayani Kyela.
Pamoja na hayo Mheshimiwa Josephine K. Manase, amewataka wanawake wote waliopata mafunzo haya, kuendelea kuwa wabunifu katika kutengeneza bidhaa zenye ubora utakaokidhi mahitaji ya hapa nchini na nje ya nchi.
" Ukimuelimisha mwanamke Umeielimisha jamii nzima, sasa kupitia sisi tuliopata mafunzo tukawe mfano wa kuigwa kwa wenzetu ambao hawajapata mafunzo haya" amesema Manase.
Pia Mheshimiwa Mkuu wa wilaya amesema mafunzo haya ni muhimu sana, kwani kilimo kimewekwa kuwa ni kipaumbele katika kujiletea maendeleo, na ndio maana tuna agenda 10/30, ambayo imeendelea kutekelezwa kwa utoaji wa ruzuku za pembejeo, kilimo cha umwagiliaji kuanzisha mashamba makubwa na mengine mengi.
Mwisho amesema wilaya ya Kyeka itaendelea kutoa ushirikiano kwa sekta binafsi ili kuhakikisha uwepo wa mazingira bora ya biashara kwa wajasiriamali wetu.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya Jamii ndugu Victor Kabuje, amewataka wanawake wote waliopata mafunzo haya kwa siku 3, kuyatumia mafunzo hayo katika kubadilisha maisha yao na atafurahi atakapoona mafunzo hayo yametoa matunda kwa wahitimu wote.
Kwa upande wake Afisa Mradi kutoka "TWCC" Bi. Cresensia Mbunda amesema lengo kubwa la kutoa mafunzo haya, ni kuwataka wanawake kwenda kuliteka soko la ndani na nje ya nchi na hasa katika Jumuiya ya Afrika ya Maendeleo ya Kusini mwa Africa ( SADC). Kwani mafunzo hayo yameshirikisha utoaji wa elimu ya biashara na fedha pia.
Lucia Mwaisumo mkazi wa Itunge kaskazini, ametoa shukrani zake za dhati kwa niaba ya wanafunzi wenzake na kusema, wanaishukuru "TWCC" kwa kuwapa mafunzo kwa siku 3 ambapo, wamejifunza mambo mengi hasa masuala ya ujasiriamali, ikiwemo Utengenezaji wa sabuni za miche, viungo kama pilau masala ambapo elimu hii inaenda kuwasaidia wao, katika kufanya kazi kwa vitendo na wanaamini kipato chao kinakwenda kuongezeka.
Mwisho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0756944794
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa