Mhe. Luhaga Joelson Mpina (katika) akizungumza na wavuvi katika mwalo wa Kafyofyo Kyela.
Haya yamezungumzwa na waziri wa wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina, alipokuwa akizungumza na wavuvi katika mialo ya ziwa Nyasa hapa wilayani Kyela, tarehe 26/10/2019.
Akizungumza na wavuvi hao katika mwalo wa Kafyofyo uliopo katika kijiji cha njisi kata ya Kajunjumele wilayani hapa, Mhe. Waziri amewataka wavuvi kuachana na mazoea ya uvuvi haramu, kwani serikali imejipanga kuanza msako mkali katika ziwa Nyasa dhidi ya wavivu wanaojishughulisha na uvuvi haramu.
Pia amesema Serikali imejipanga kuanza doria hiyo siku ya tarehe 27/10/2019, kwani katika ziara yake katembea na watalam kutoka wizarani kwake, ambao watashughulikia swala hilo mara moja.
Aidha Mhe. Luhaga Joelson Mpina, ameahidi kuleta vifaranga vya samaki katika mabwawa yote ya samaki yaliyopo katika ziwa Nyasa, hii ni kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa samaki.
Hata hivyo Mheshimiwa waziri, amewatoa wasiwasi wavuvi wote kwamba, haitapita wiki moja kuanzia sasa, wavuvi wote wataanza kupewa elimu ya uvuvi bora na salama, ili waweze kuvua kwa vikundi na baadae kuweza kupata mikopo kutoka serikalini.
Akizungumza kwa niaba ya wavuvi ndugu Andrew Mwaisemba amesema, ni kweli wavivu wengi walikuwa wakifanya uvuvi haramu katika ziwa Nyasa, na kusababisha ziwa kukosa samaki kabisa kwa sasa. Na alimwomba Mhe. Waziri kutatua changamoto za miundo mbinu mibovu, kuwawekea sehemu za kupumzika na kupewa mikopo.
Mwisho Mhe. Waziri alipata fulsa ya kutembelea katika kata ya Matema na kuzungumza na wavuvi wa maeneo hayo pia.
Waziri wa wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Joelson Mpina akiwasili katika mwalo wa Kafyofyo uliopo kata ya Kajunjumele wilayani Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa