Halmashauri ya Wilaya ya Kyela yatoa elimu juu ya umuhimu wa Baba na Mama kwenda kliniki pamoja, elimu hii imetolewa tarehe 4/06/218 katika viwanja vya Godauni Ipinda.
Akizungumza na Wananchi katika hafla iliyoandaliwa na shirika la UNICEF kupinda BBC World, Kaimu Mratibu wa huduma za mzazi na mtoto Bi.Atupokigwe Gidioni alisema.
Kuna faida nyingi za mama mjamzito kwenda kliniki mapema, ikiwemo kupata huduma muhimu za awali, kujua ukuaji wa mtoto akiwa tumboni, kupata dawa muhimu za kuzuia maralia na minyoo, kuongezewa damu pamoja na kupewa chandarua kwa ajiri ya kuzuia Mbu.
Mwisho alitoa ushauri kwa jamii nzima ya Kyela kwa Wazazi kuwahi mapema kliniki ili kuepuka madhara mbalimbali.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa