Mwenyekiti wa chama cha Msalaba Mwekundu Kyela, ndugu Obed Elia Mwalusaka amekabidhi balakoa 150 katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kyela jana tarehe 28/05/2020.
Akikabidhi balakoa hizo mwenyekiti wa chama cha msalaba mwekundu wa kata ya Itunge wilayani Kyela amesema, chama kimeguswa sana kwa namna ambavyo wilaya ya Kyela inavyotekeleza maelekezo ya kujikinga dhidi ya virusi vya corona. Hivyo msaada huu wa balakoa 150 umelenga kuwafikia wananchi wote wenye kipato cha chini.
Akipokea balakoa hizo mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe.Claudia U.Kitta, ametoa shukrani zake za dhati na kusema kwamba, tunathamini sana michango inayotolewa na chama cha msalaba mwekundu wilayani Kyela. Chama kimekuwa kikitoa ushirikiano kwa serikali katika kusaidia majanga mengi kwa mfano mafuriko. Pia Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Ndugu Ezekiel H. Magehema amekishukuru chama na kuomba baadhi ya balakoa hizo ziende kusaidia wanafunzi wanaofungua shule tarehe 01/06/2020.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa