Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, wamefanya Baraza la kazi la robo ya nne leo 18/08/2023, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela.
Baraza hilo limehudhuriwa na waheshimiwa madiwani wote, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Wakuu wa Idara mbalimbali na Vitengo.
Akifungua baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono amewasifu wataalamu kwa kufanya kazi vizuri kwa robo zote nne.
Aidha amewapongeza wataalamu kwa usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato na matumizi na kuifanya Halmashauri kupata Hati Safi.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Bi. Florah A. Luhala, amezipokea pongezi hizo kwa dhati na kuahidi kuendelea kuchapa kazi.
Aidha ametumia Baraza hilo kujitambulisha kwa waheshimiwa madiwani kwani baraza hilo, ni la kwanza kuhudhuria tangu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela.
"Naomba nijitambulishe kwenu, lakini pia ninawakaribisha Ofisini kwangu mda wowote ili kujadiliana changamoto yoyote inayojitokeza" amesema Luhala.
Katika Baraza hilo waheshimiwa Madiwani wamepata nafasi ya kuwasilisha taarifa za kazi kutoka katika kata zao.
Mwisho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa