BARAZA la madiwani wa halmashauri ya wilaya Kyela, limeadhimia kumuandikia ombi maalum, Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, ili aweze kuwasaidia kuhakikisha maboma 14 yaliyojengwa na wananchi, zikiwemo zahanati yanakamilishwa.
Limesema wananchi wamejitoa nguvu, muda na mali zao kuhakikisha maendeleo yanasonga mbele katika wilaya hiyo, hivyo katika eneo hilo ni vizuri baraza hilo kwa kushirikiana na wataalam wapeleke ombi maalum kwa Mkuu wa nchi.
Hayo yalijiri katika kikao cha baraza la madiwani,kupitisha rasimu ya bajeti ya mwaka 2023/2024, kwa ajili ya utekelezaji wa matumizi ya halmashauri ya wilaya Kyela, kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa halmashauri, Katule Kingamkono, alisema bajeti yao ina kiasi cha sh.bilioni 5.071,kutoka sh.bilioni 4.681, ikiwa ni ongezeko la asilimia 8.13, ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2022/23.
Kingamkono alisema madiwani, wenyeviti wa vijiji na vitongoji pamoja na wananchi, wamekuwa na muitikio mkubwa wa uainzishwaji wa miradi mingi ya maendeleo, kutokana na nguvu kazi zao na mpaka sasa wanayo maboma 14 yaliyo jengwa.
“Tunaposema maboma 14 unazungumzia zaidi ya sh.milioni 900 hadi sh.bilioni moja na kidogo,lakini ukiangalia bajeti yetu tuliyoipitisha leo katika masuala ya afya tunazo sh.milioni 320, hivyo hapa tunazungumzia upatikanaji wa zaidi ya sh.milioni 600 hadi 800” alisema Kingamkono.
Aliongeza hivyo wameona serikali kuu ndiyo mlezi wao, na Rais Dk.Samia miongoni mwa maeneo aliyoelekeza nguvu kubwa ni katika afya, hivyo baraza lake limeona wawe na ombi maalum ili maboma yaliyopo yaweze kukamilishwa na wananchi waendelee kupata huduma.
Awali, diwani wa kata ya Itungi, Dickson Mwalukama, alisema kumekuwa na maboma mengi yakiwemo ya zahanati yaliyojengwa,na kuwashukuru wananchi pamoja na wenyeviti wa vitongoji na vijiji, ambao wamekuwa karibu na wananchi.
Alisema pamoja na maboma mengi yaliyopo, anao uhakika kwamba fedha waliyonayo ni ndogo, na ili waweze kuwaunga mkono wananchi wao kwa kazi kubwa wanayoifanya, kwa kushirikiana na wenyeviti wa vitongoji, vijiji pamoja na madiwani.
“Kupitia baraza hili naomba kwamba ni vizuri tungeandaa ombi maalum, kwa Rais wetu Dk.Mama Samia,ambaye ni msikivu nina uhakika tukipeleka maombi
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa