Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono ameongoza mkutano wa Baraza la kufunga Mwaka 2023/2024 la Waheshimiwa madiwani, katika ukumbi wa mikutano wa Halmshauri tarehe 09/09/2024.
Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri Bi. Flora A. Luhala, Katibu tawala (W) Bi. Sabrina Houmud, taasisi mbalimbali za Serikali, Viongozi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), wataalam kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, pamoja na Wananchi.
Aidha katika Baraza Hilo umefanyika uchaguzi wa kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya ya Kyela, ambapo, Mhe. Ambakisye Njerekela, ameibuka mshindi kwa kura za wajumbe 36 waliopiga kura.
Pia kulikuwa na uundwaji wa kamati za kudumu za Baraza kwa Mwaka 2024/2025, ikiwemo kamati ya Elimu na Afya, kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, kamati ya Lishe, kamati ya Maadili na kamati ya Uongozi Fedha na Mipango.
Akizungumza kwa niaba ya Mhe. Mkuu wa wilaya ya Kyela, Katibu Tawala (W) Bi. Sabrina Houmud, amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kuanzisha na kuendeleza miradi ya maendeleo wilayani Kyela.
Pamoja na hayo Bi. Sabrina amempongeza Mhe. Ambakisye Njerekela kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya ya Kyela, pia amesisitiza kuendelea kudumisha ushirikiano uliopo baina ya Wanakyela.
Sambamba na hilo amewashukuru Waheshimiwa madiwani, kwa ushirikiano mzuri waliouonesha wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, uliopokelewa tarehe 28/08/2024, wilayani Kyela.
Kuelekea katika uchaguzi mdogo wa Serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 27/11/2024 Bi. Sabrina Houmud, amewaomba Waheshimiwa Madiwani na wataalam mbalimbali kuendelea kutoa elimu na ushirikiano ili kuhakikisha elimu ya kujitokeza kupiga kura inamfikia kila mwananchi.
Awali Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya ya Kyela Mhe. katule G .Kingamkono, amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Kyela.
Hata hivo Mhe. Katule ameendelea kutoa ufafanuzi wa utekelezaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii katika Halmshauri ya wilaya ya Kyela kwa mwaka wa fedha 2023/2024, ikiwemo ukusanyaji wa mapato kwa 133%.
Akitoa salamu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Katibu mwenezi wa Chama Ndg. Emmanuel Mwamulinge, amewapongeza waheshimiwa Madiwani na wataalam kwa ushirikiano mzuri na Chama Cha Mapinduzi na kufanikiwa kiendelea kuleta maendeleo wilayani.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa