Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kyela Mhe. Emmanuel K. Bongo ameongoza mkutano wa baraza la wenyeviti la robo ya 4 ya mwaka 2023/2024, katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Mji Mdogo tarehe 21/8/2024.
Mkutano huo umehudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya wilaya ya Kyela Bi.Florah A. Luhala, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani, wataalamu kutoka ngazi ya mkoa na wilaya.
Akijibu maswali ya papo kwa papo yaliyoulizwa na baadhi ya wajumbe ikiwemo suala la malamlaka ya mji mdogo wa Kyela kurasimishwa kua halmshauri ya mji Mhe. Mwenyekiti amesema"
"Taratibu zote zinapangwa na Serikali na yenyewe ndio inaamua mamlaka kua halmshauri ya mji, hivyo utekelezaji upo kwani tunakidhi vigezo vya mamlaka yetu kua halmshauri ya mji tundelee kuvuta subira kusubiri taratibu za kiserikali.
Katika mkutano huo Mhe. Mwenyekiti amesema mamlaka imeendelea kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa mapato ndani ya robo ya nne hadi kufikia 82%, kuimarisha miradi ya maendeleo ikiwemo utoaji wa fedha kwa haraka kwa ukarabati wa soko la olofea, ujenzi wa jengo la kupumzikia abiria stendi kuu ya mabasi Kyela, uboreshaji wa miundombinu ya barabara kata ya Serengeti.
Aidha Mhe. Bongo amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya wilaya ya Kyela Bi. Florah A. Luhala kwa ushirikiano mzuri baina ya Halamashauri na Mamlaka hata kupelekea ukamilishaji wa miradi ya maendeleo wilayani Kyela.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Kyela Ndg.Gerald Mlelwa, amewaomba viongozi waliohudhuria mkutano huo kuhamasisha wananchi waliopo katika maeneo yao, kujitokeza kwa wingi kupokea Mwenge wa Uhuru unaotarajia kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo tarehe 28/8/2024.
Sambamba na hilo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg.Gervas Deus ameishukuru Mamlaka ya Mji Mdogo, kwa ushirikiano mzuri na Chama Cha Mapinduzi, pia amewaomba viongozi kuhamasisha wananchi, kujiandaa na uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwezi wa 11 mwaka huu.
Awali Meneja msaidizi huduma ya mlipa kodi mkoa wa Mbeya Ndg. Stephen Kauzen ameipongeza Halmshauri ya wilaya ya Kyela, kwa ukusanyaji mzuri wa mapato kwa miaka 3 mfululizo, pia amewaomba viongozi kuhamasisha wananchi kuwa na "taxpayer" identification number (TIN NUMBER) zitakazowasaidia kufanya shughuli zao ikiwemo biashara bila usumbufu.
Vilevile Kauzen amemuagiza Afisa elimu wa mapato ngazi ya mkoa kuja kutoa elimu kwa wananchi wilaya ya Kyela, juu ya umuhimu wa ukusanyaji mapato.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Hospital ya wilaya ya Kyela, Dkt. Saumu Kumbisaga amewaomba wananchi kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa kipindupindu.
Ikiwemo kufanya usafi wa mazingira, pia ameongeza, kusema kuwa serikali inapambana kudhibiti ugonjwa huu kwani mpaka sasa wameweza kutoa kinga (vidonge vya kuua wadudu) katika shule 161, pamoja na kufunga biashara ya chakula kwa baadhi ya migahawa isiyokidhi vigezo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa