Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Katule G. Kingamkono akifungua kikao cha Baraza, katika Ukumbi wa mikutano wilayani Kyela.
Mbunge wa jimbo la Kyela Mhe. Ally Mlaghila Jumbe akiwa katika kikao cha Baraza la Waheshimiwa Madiwani wilayani Kyela.
Haya yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono alipokuwa akifungua kikao cha baraza maalumu la kuwakilisha hesabu za mwisho za mwaka 2022/2023.
Akifungua kikao hicho leo 29/08/2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, Mheshimiwa mwenyekiti amesema;
Tunawapongeza watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela kwa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa, uaminifu na jitihada kubwa hadi kufikisha ukusanyaji wa mapato kwa 107% kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Amesema mafanikio haya, yametokana na jitihada kubwa wanazozifanya watumishi wetu pamoja na ushirikiano uliopo baina ya viongozi wa ngazi zote katika wilaya.
Aidha Mhe. Katule G. Kingamkono ametoa shukrani kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kutuletea fedha kutoka Serikali kuu, kiasi cha shilingi 35,842,014,652.43/= zilizotusaidia katika kutekeleza miradi ya maendeleo na shughuli mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Nae Mbunge wa jimbo la Kyela Mhe. Ally Mlaghila Jumbe ametoa pongezi kwa watumishi juu ya uadilifu na kufanya kazi nzuri kwa kila idara na kitengo.
Pia ametoa shukrani zake za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani, kwa kutoa fedha ambazo zinajenga madarasa kila Mwaka na kuondoa kero ya wananchi kudaiwa michango katika ujenzi wa shule au madarasa.
Pamoja na hayo Mhe. Mbunge ameahidi kuendelea kupambana na kuhakikisha maboma yote ya shule na zahanati ambayo hayajaezekwa yanaezekwa kwa maandalizi ya umaliziaji.
Aidha ametoa pongezi kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (W) kwa kutusimamia na kutuongoza vema.
Awali Afisa tarafa ya Unyakyusa ndugu, Herry william, ametoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa wilaya Mhe. Josephine Manase, amesema;
Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ya Kyela, amesisitiza suala la kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata zetu, Pia amepongeza ushirikiano uliopo baina ya viongozi wote wa wilaya na ameomba ushirikiano huo uzidi kudumishwa.
Halmashauri ya wilaya ya Kyela imeweza kukusanya mapato ya shilingi 5,003,013,553.09/= sawa na 107% zaidi lengo la kukusanya shilingi 4,681,366,320.00/= kwa mwaka 2022/2023.
Mwisho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa