Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mhe.Katule G. Kingamkono ameongoza Baraza la robo ya pili katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri tarehe 6.2.2024.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela,Katibu Tawala Bi. Sabrina Hamoud amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta Fedha kwa ajili ya kukamilisha na kuendeleza Miradi ya maendeleo.
Pia Amempongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupitishwa na mkutano Mkuu wa (CCM) kuwa Mgombea wa Urais wa Tanzania kwa Mwaka 2025.
Aidha Katibu Tawala amewapongeza Wah. Madiwani pamoja Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi kwa ushirikiano na ukusanyaji wa Mapato na kufikisha 98% zilizovuka malengo ndani ya robo ya pili.
Katibu Tawala amewataka Wah.Madiwani kwa kushirikiana na Waratibu Elimu pamoja na Maafisa Elimu kuwahamasisha Wazazi wenye Watoto waliofaulu kujiunga na masomo ya Sekondari ili wakaendelee na Masomo kwani mpaka sasa wanafunzi walioripoti shuleni ni 78% tu.
Kuhusiana na Mikopo ya 10% inayotolewa kwa Wanawake Vijana na watu wenye Ulemavu Bi. Sabrina amempongeza Mkurugenzi na Ofisi ya maendeleo ya Jamii kwa ufuatiliaji na utoaji mzuri wa Elimu kwa Wananchi wenye vigezo vya kupata Mikopo hiyo itakayoanza kutolewa hivi karibuni.
Mhe.Katule amesema kuzidi kwa malengo ya Mapato hayo yaliyofikia 98% ndani ya robo pili amemwagiza Mkurugenzi kununua mitambo ya kutengeneza Barabara( Greda,Rolla) kupunguza na kuondoa changamoto yenye ubovu Miundombinu kwa baadhi ya Kata, Vijiji na vitongoji vyenye changamoto hiyo.
Hali kadhalika Mhe .Mwenyekiti amesema Halmashauri imeandaa mkakati kwa kila Kata Vijiji na Vitongoji kuendeleza Zao la Kokoa kwa kugawa Miche kwa Wananchi ili kuimarisha Uchumi wa Wananchi na Wilaya kwa ujumla.
Akijibu maswali ya Papo kwa hapo yaliyoulizwa na Wah.Madiwani ikiwemo ujenzi wa Soko kwa wajasiriamali wadogo (wauza matunda) Mhe. Katule amesema Halmashauri ipo kwenye mpango wa kujenga jengo hilo ili kuwatengenezea mazingira bora ya biashara.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa