Benki kuu ya Tanzania (BOT) tawi la Mbeya wameongoza semina, kwa wadau juu ya uwekezaji kwenye dhamana za Serikali 2024/2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmshauri tarehe 03/09/2024.
Semina hiyo imehudhuriwa na wadau mbalimbali, wakiwemo, wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri, Taasisi za serikali pamoja na wananchi.
Akiongea kwa niaba ya Mhe. Josephine Manase, Mkuu wa wilaya ya Kyela Ndg. Rowllens Kabuje, amewashukuru wataalam kutoka Benki Kuu kwa kutoa elimu juu ya uwekezaji, kwenye dhamana za Serikali katika wilaya ya Kyela, pia amewasihi wadau mbalimbali kujiunga na huduma hiyo, ili kuachana na aina ya mikopo kandamizi.
Akitoa elimu kwa wadau waliohudhurua semina hiyo Ndg. Luther Luvanda ameeleza namna ya ushiriki katika dhamana za serikali ikiwemo dhamana za mda mfupi kuanzia miezi 3, mpaka mwaka 1 pamoja na dhamana za mda mrefu kuanzia miaka 2 na kuendelea.
Aidha Ndg. Luvanda ameeleza faida za dhamana za serikali kwa wawekezaji ikiwemo viwango vya riba zinazoridhisha, kugharamia bajeti, kupata fedha za kuendesha miradi ya maendeleo pamoja na kutoa fursa za uwekezaji.
Vilevile Ndg. Luther Luvanda amefafanua vigezo vitakavyomuwezesha mdau kujiunga na huduma hiyo ikiwemo, mwananchi mwenye umri wa miaka 18, kitambulisho cha Taifa, Tax Payer Identification Number ( TIN NUMBER), na kitambulisho cha mpiga kura.
Mwisho wadau walipata fursa ya kuuliza maswali yaliyojibiwa na mtaalam kutoa Benki Kuu kwa ufafanuzi uliwalidhisha wadau wote.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa