Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Claudia U. Kitta amezindua bodi mbili za maji yaani Bodi ya maji ya mji mdogo Kasumulu na Bodi ya maji ya mji mdogo Ipinda julai 6 2018.
Akizindua bodi hizo Mkuu wa Wilaya amewataka Wajumbe wa bodi za maji zilizoundwa kufanya kazi kwa lengo la kuwahudumia Wananchi, pia amewataka Wananchi kulinda na kuvitunza vyanzo vyote vya maji vilivyopo Kyela, lakini amesisitiza swala la ulipaji wa bili za maji kwa wakati kama afanyavyo yeye.
Amesema kuna baadhi ya ofisi za umma zinadaiwa bili za maji na zimekuwa zikichelewesha malipo ya bili, hivyo kwa uzinduzi wa bodi hizi anaamini zitafanya kazi kwa kasi ili kuhakiki bili za maji zinalipwa kwa wakati kutoka kwa Wananchi na ofisi za serikali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe. Hunter Mwakifuna aliwaambia wajumbe kwamba swala la maji haliitaji itikaji, tukiingiza siasa katika swala hili tutauwa watu, fanyani kazi wajumbe wote mlioteuliwa kuunda bodi hizi.
Aidha Meneja wa maji mji mdogo Kasumulu bi. Atunosyege A. Mwakang'ata alitoa changamoto mbalimbali zinazoukabili utoaji huduma za maji Kasumulu zikiwemo,
Uchakavu wa miundo mbinu ya maji, kutokuwa na eneo la kujenga ofisi, kutokuwa na eneo la kutililisha maji taka, ujenzi holela wa kujenga juu ya miundo mbinu ya maji pamoja na matumizi ya miundo mbinu ya teknolojia ya zamani katika chanzo cha maji cha mto Mwega.
Aidha lengo kuu la Mamlaka ya maji Kasumulu ni kutoa huduma bora ya maji kwa wakazi 19,214 ila kwa sasa wanaopata maji kwa shida shida ni wakazi 6,980.
kwa upande wa Ipinda lengo ni kuwafikia wakazi 11,750 ila kwa sasa ni wakazi wa kanga ambao ni 8,770 tu.
Mwisho tunapenda kutoa pongezi kwa Serikali ya awamu ya tano kwa jitihada inazozifanya kuondoa kero za Wananchi wake Tanzania.
Meneja wa maji wa mji mdogo Kasumulu Bi. Atunosyege A. Mwakang'ata akipokea cheti chake cha kuteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya maji Kasumulu.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa