Uongozi wa Kata ya Mwanganyanga wilayani Kyela, umekabidhi choo cha kisasa kwa Mamlaka ya Mji mdogo wa Kyela, leo tarehe 01/02/2023, kilichokuwa kinakarabatiwa katika eneo la soko la wakulima lililopo eneo la Olofea hapa wilayani Kyela.
Makabidhiano hayo yamefanyika mara baada ya uongozi wa kata ya Mwanganyanga kwa kupitia kamati ya ukarabati wa choo hicho kujiridhisha na ukamilifu wa ukarabati huo kukamilika.
Akitoa taarifa kabla ya makabidhiano ya choo hicho, Mtendaji wa kata ya Mwanganyanga ndugu Mjemaso A. Mwambungu amesema,
Ukarabati wa choo hicho ulianza tarehe 25/11/2022 mara baada ya Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji mdogo ndugu, Gerald Mlelwa kutenga na kuingiza kiasi cha shilingi 20,000,000/= katika akaunti ya kata, na kuanza ukarabati kwa njia ya "force account", hadi kukamilika kwake.
Aidha makamau mwenyekiti wa Mamlaka ya mji Mdogo wa Kyela Mheshimiwa Michael Mwakibinga, ameridhishwa na ukarabati wa choo hicho na kukubali kukipokea kwa matumizi ya wananchi.
"Niwapongeza viongozi, kamati ya ujenzi pamoja na wananchi wote walijitolea katika ukarabati wa choo hichi bila malipo yoyote na hatimae kukamilisha ukarabati huu" amesema Mhe. Mwakibinga.
Pamoja na hayo Mhe. Mwakibinga ameahidi kukitunza choo hicho kwani ni chanzo kizuri cha Mapato kwa Mamlaka ya mji mdogo, lakini pia choo hicho ni msaada si kwa wafanyabiashara wa soko la wakulima tu bali kwa wananchi wote wa wilaya ya Kyela.
Hata hivyo diwani wa kata ya Mwanganyanga Mhe. Alex Mwinuka, alimaarufu kwa jina la Bonge, ameiomba Mamlaka kuendelea kulipia umeme katika choo hicho ili kuendelea kupata huduma ya maji katika choo hicho, kwani huduma ya maji inapatikana kwa nishati ya umeme chooni hapo.
Lakini pia aliwasihi wananchi wote kuendelea kukitunza choo hicho ili kiweze kudumu kwa mda mrefu zaidi.
Miundombinu ya maji iliyopo katika choo cha kisasa kilichopo katika soko la wakulima Olofea hapa wilayani Kyela.
Bafu lililopo katika choo cha kisasa katika soko la wakulima Olofea hapa wilayani Kyela.
Mwisho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa