Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Josephine Manase amelitaka shirika la umeme TANESCO Kyela kwenda kutoa elimu ya kutumia simu za mkononi, ili mteja mpya aweze kulipa na kupata huduma ya kuunganishwa na huduma ya umeme.
Amewataka wataalam wa TANESCO Kyela, hadi kufikia tarehe 18/05/2023 wawe wamefika katika kata ya Njisi kutoa elimu, Ikiwa ni utatuzi wa moja ya kero iliyowasilishwa na baadhi ya wananchi wa kata ya Njisi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika tarehe 16/05/2023 hapa wilayani Kyela.
Aidha amesema tunamshukuru Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuiletea maendeleo ya wilaya, tunaona miradi ya maendeleo ikitekelezwa kila upande.
Kuhusiana na suala la umeme wa REA, Mhe. Josephine, amewaambia wanaNjisi kuwa kata ya Njisi ipo ndani ya Mamlaka ya mji mdogo ambapo, wananchi wote wanaoishi ndani ya mamlaka wanatakiwa kulipa shilingi 320,000/= ili kuunganishwa na huduma ya umeme.
Kwa huruma ya Mhe. Rais. Dkt Samia Suluhu Hassan, ameunda timu ya kufanya tathimini katika vitongoji ili kubaini maeneo yote ambayo yatafanyiwa tathimini na kujiridhisha kupeleka umeme wa REA. Hivyo wananchi wawe na subira mpango huo utakamilika kila mwananchi atapata umeme wa REA katika maeneo teule.
Mhe. Mkuu wa wilaya, amekili kwamba maji ni changamoto kwa wilaya ya Kyela, lakini kuna miradi ya maji inayotekelezwa hadi sasa ingawa bado haijakamilika.
Kero ya baadhi ya wananchi kujichukulia sheria na kujenga nyumba katika mipaka ya barabara, Mhe. Mkuu wa wilaya amewataka wananchi wote wawe walinzi kwa wananchi wenzao, ambao wanajenga katika maeneo ya barabara na kutoa taarifa mapema pale inapobainika.
"Ninatoa onyo kwa wenyeviti wa vitongoji wote, Kwa muda wote ambao nitakuwepo hapa, nisisikie mwenyekiti ameuza eneo bila kuwa na ushahidi wa kutosha, tutagombana".amesema Mhe. Josephine.
Mwisho amesema, Leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya Familia duniani, amewakumbusha wazazi kuwalea watoto katika malezi bora, amesema tusipo walea watoto katika maadili mema, kizazi kijacho kitakuwa ni kizazi cha ajabu.
Aliendelea kusema jukumu la kulea watoto ni la Baba, Mama na jamii nzima, hivyo amewaomba wazazi kujenga familia zenye misingi bora. Pia amewataka kutoa taarifa wanapoona mtu yeyote anakwenda tofauti na maadili yetu.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, ndugu Ezekiel H. Magehema amesema, Hatuna budi kumpongeta Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kwa kutuletea miradi mingi katika wilaya yetu, Na kuhusiana na suala la nyumba za watumishi amewaomba wananchi kuandaa maeneo kwani, nyumba za watumishi zitajengwa na zitajengwa kwa awamu.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa