Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhr.Josephine Manase amefungua mafunzo ya kuongeza virutubishi kwenye unga wa mahindi tarehe 16.9.2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Akizungumza na wadau wa Lishe katika ufunguzi wa mafunzo hayo Mhe. Manase amesema mafunzo haya yanalenga kuleta uelewa kuhusu Sheria mpya za viwango zilizotolewa na Serikali tarehe 15.11.2024 juu ya ufafanuzi wa kanuni za uongezaji wa virutubishi kwenye chakula.
Aidha Mhe.Manase amewataka wadau wote wa Lishe kuwa na ushirikiano kati yao na kuwa mabalozi wazuri, hivyo wanapaswa kuzingatia utekelezaji wa Sheria zote uongezaji wa virutubishi kwenye chakula ili kuepukana na upungufu wa viini Lishe muhimu kwenye jamii zetu.
Akiendelea kusisitiza umuhimu wa Lishe shuleni Mhe.Manase amesema ni muhimu kwa kila mwanafunzi kupata chakula cha mchana awapo Shuleni hivyo amewataka walimu kuweka mikakati na ajenda za kudumu juu ya kutoa Elimu kwa Wazazi kuhusu Lishe ili waweze kutoa mchango wa chakula.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa