Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe Josephine Manase amefanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kijiji cha Katumba Kata ya Katumbasongwe tarehe 22.7.2025.
Miongoni mwa kero zilizotajwa ni pamoja na kuwepo kwa michango, kuendelea kwa matumizi ya Nishati chafu pamoja na changamoto ya Ugonjwa kwenye mazao.
Akitatua kero ya matumizi ya nishati chafu Mhe. Manase amesema Serikali ipo inafanya tathimini namna ya kuboresha upatikanaji wa nishati safi kwa Wananchi kama kuwepo kwa umeme kwenye Vitongoji na Vijiji ili Kila Mwananchi aweze kuipata Kwa gahalama nafuu zaidi kulingana na kipato Cha Kila mtu, kwahiyo itakuwa rahisi kuunga Mkono juhudi za Mhe. Rais juu ya matumizi ya nishati safi.(alisema Mhe: Manase)
Aidha Mhe. Manase amemuagiza Mwenyekiti wa Kitongoji kufanya vikao vya kukubaliana na Wananchi wake juu ya michango yoyote inayojitokeza kwenye Kijiji kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Sambamba na hayo Mhe.Mkuu wa Wilaya amewataka Maafisa Ugani kuweka utaratibu wa kutembelea Wananchi husani wakulima kwa ajili ya kutoa ushauri na kubaini changamoto zao na kuzifanyia utatuzi.
Katika jitihada za kuunga mkono juhudi za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya suala la Elimu bure Mhe.Manase amewahimiza Wazazi wenye watoto Shuleni kuchangia chakula ili kuimarisha Afya na akili ya mtoto,kuondoa matabaka, pamoja na kujenga ushirikiano mzuri na wenzake pindi awapo Shuleni.
Mhe.Manase amewataka Vijana wenye Elimu walio Mtaani kujiunga na mifumo inayotangaza ajira ili waweze kujua nafasi mbalimbali za kazi zinazotolewa na serikali.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa