Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyela imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata ya Katumbasongwe, tarehe 29 Julai 2025.
Katika ziara hiyo, kamati ilitembelea miradi ya sekta ya afya, kilimo na elimu, ambayo inatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali Kuu, Halmashauri, wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Mojawapo ya miradi hiyo ni ujenzi wa Zahanati ya Itekenya Mpunguti, ambapo fedha zimetoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo michango ya wananchi ni Shilingi milioni 27, na fedha kutoka Serikali Kuu ni Shilingi milioni 30. Hadi sasa mradi huo umefikia hatua ya upigaji ripu nje na ndani, na unatarajiwa kuboresha huduma za afya kwa wakazi wa eneo hilo.
Kamati pia ilikagua ujenzi wa nyumba ya Afisa Ugani, ambapo mradi umegharimu jumla ya shilingi milioni 50 zilitolewa kutoka vyanzo mbalimbali. Ikiwemo Wizara ya Kilimo ilichangia Shilingi milioni 40, lakini pia Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kupitia Mapato ya ndani ilitoa shilingi milioni 9,364,000 huku wananchi wakichangia Shilingi 350,000.
Katika sekta ya elimu, kamati ilitembelea ujenzi wa bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Katumbasongwe. Ambapo kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyela imetoa kiasi cha shilingi milioni 50 na ujenzi umefikia hatua ya upigaji ripu. Kukamilika kwa bweni hili kutasaidia kupunguza changamoto kwa wanafunzi wanaotembea umbali mrefu kufuata masomo yao.
Aidha, kamati ilikagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Isaki, ambapo mradi unagharimu Tsh 125,000,000 mpaka kukamilika kwake mpaka sasa zaidi ya shilingi Milioni 70 kutoka vyanzo mbalimbali zimetolewa, Ikiwemo michango ya Wananchi walichangia shilingi Tsh.16,519,000 Halmashauri ya Wilaya ya Kyela imetoa shilingi milioni 13, Fedha kutoka Serikali Kuu ni shilingi milioni 30, Mamlaka ya Bandari shilingi milioni 5,940,000 Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata shilingi elfu 30, wadau wengine shilingi milioni 2,258,000 na Mfuko wa Mbunge shilingi milioni 2,500,000. Mradi huu unatarajiwa kuboresha huduma za afya kwa wakazi wa Kijiji cha Isaki kwa kuwapatia huduma ya haraka na ya karibu.
Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Adv. Florah A. Luhala, amewataka viongozi wa kata kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa na Serikali na wadau mbalimbali zinasimamiwa kikamilifu ili miradi ya maendeleo ikamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa