Hayo yamethibitisha na mratibu wa mfuko ya afya ya jamii ulioboreshwa ndugu Nelusigwe S. Mwakigonja, alipokuwa akifanya usajili wa kaya yenye jumla ya watu 6 katika eneo la KYECU lililopo hapa wilayani Kyela, siku ya ijumaa tarehe 16/08/2019.
Mratibu huyo wa mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa ameweza kutoa ufafanuzi kuhusu kuchangia kiasi hicho cha shilingi elfu 30000,kwa kaya 1 yenye jumla ya watu 6 yaani Baba, Mama pamoja na watoto 4, ili kuweza kufanikisha zoezi hili la usajili ambalo linafanywa kwa wananchi wote hapa wilayani.
Aidha Mratibu wa mfuko wa afya wa jamii ametoa wito kwa jamii nzima kuwa afya ndio msingi kwa maendeleo ya jamii, hivyo ni jukumu letu sisi wananchi kutambua umuhimu wa afya zetu.
Pia amewaasa wananchi kuwa na tabia ya kujihudumia wenyewe ili kuwa na jamii endelevu kupitia mfuko wa bima ya afya ya jamii (ICHF) na kusisitiza kuwa walengwa wa mfuko huu ni wananchi wote.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa