Haya yamezungumzwa na Mhe. Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Katule Kingamkono alipokuwa akifungua mafunzo ya watendaji wa vijiji 93 na kata 33 wilaya ya Kyela, mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi mkubwa wa halmashuri ya wilaya ya Kyela tarehe 14/04/2021.
Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo Mhe. Mwenyekiti amesema katika swala la mapato wilaya ya Kyela ipo mikononi mwa watendaji, sababu unapozungumzia mapato ya halmashauri basi tunaanza na watendaji katika ngazi ya kijiji na kata. Na ndio maana tumeamua kufanya mafunzo haya ili kila mtendaji ajitambue na atambue nini cha kufanya katika mazingira yake ya kazi.
Pia Mhe. Mwenyekiti alitoa pongezi kwa watendaji wote ambayo wamekusanya mapato kwa kasi kubwa hadi kuifanya wilaya ya Kyela kuongoza mkoa kwa ukusaji mapato kwani hadi sasa tumefika asilimia 78.96, kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa kwa muda huu tangu halmashauri ianzishwe.
Pamoja na hayo, Mheshimiwa mwenyekiti wa halmashauri amewataka watendaji wote kutoa taarifa za mapato na matumizi katika mikutano yao, ili kuwaweka wazi wananchi kujua mapato na matumizi ya pesa zao, Hata hivyo amewataka watendaji kupeleka benki pesa wanazozikusanya . Na alimaliza kwa kuwaahidi watendaji kwamba hakuna mtendaji yoyote atakaeonewa kiutumishi endapo kama atafuata taratibu ,kanuni na sheria za utumishi.
Aidha Mhe. Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji mdogo Emmanuel Bongo alisema, viongozi wasitumie majungu katika kuwaongoza watendaji, kwani watendaji ndio waliosimamia vizuri uchaguzi hadi kupata viongozi imara hivyo ni vyema kurudisha fadhira kwao.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu Ezekiel Magehema aliwataka watendaji waende wakasimamie ukusanyaji wa mapato katika vijiji vyao na kata zao na kuondokana na hali ya kuwa walalamikaji, amewataka viongozi hao waende wakafanye kazi.
Aidha alisema hatashindwa kumuajibisha mtendaji yeyote yule ambae atafanya kazi kinyume na utaratibu,sheria na kanuni za kazi mara tu baada ya mafunzo haya. Pia alitoa pongezi kwa watendaji wote waliofanya kazi kwa bidii na hadi kuifanya wilaya kuwa juu katika kukusanya mapato katika mkoa wetu. Mwisho aliwatakia mafunzo mema watendaji wote wa vijiji na kata waliohudhulia mafunzo hayo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa