Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase tarehe 26/01/2023, ametembelea eneo ambalo shule ya wasichana "Kokoa Girls" inatarajiwa kujengwa katika kata ya Nkokwa kijiji cha Sinyanga hapa wilayani Kyela.
Katika ziara yake Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ya Kyela ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Bi. Florah Luhala akiwa na baadhi ya Wakuu wa Idara na vitengo.
Akiongea na wananchi wa kata ya Nkokwa Mhe. Manase amesema, shule ya Kokoa Girls itachukua wanafunzi ndani na nje ya wilaya ya Kyela, hivyo amewataka Wanankokwa kuanza haraka kufanya usafi katika eneo la ujenzi kwani fedha za mradi zipo. Pia anewashukuru Wanankokwa kwa kujitolea eneo la ujenzi kwani hayo ndiyo maendeleo ya kweli.
Aidha ametoa Shukrani zake za dhati kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera, ambae ameendelea kuwa mbunifu katika kuanzisha na kusimamia, miradi mbalimbali katika wilaya ya Kyela.
Vilevile Mhe. Mkuu wa wilaya ya Kyela ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha anapeleka wataalam kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa shule, ikiwemo kuhakikisha maji yanapatikana kwa wakati katika eneo la mradi.
Halmashauri ya wilaya ya Kyela inatarajia kuanza na ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa ofisi 1 na vyoo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa