Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela wametembelea na kukagua Miradi 18 ya maendeleo ikiwa ni katika ziara za kawaida za kila robo ya mwaka, ukaguzi uliofanyika tarehe 30 na 31/07/2021 na kumalizika tarehe 04/08/2021 hapa wilayani Kyela.
Kwa kupitia kamati ya Elimu, Afya na Maji, Waheshimiwa madiwani wameweza kukagua miradi ya ujenzi wa zahanati ya Kapamisya iliyopo katika kata ya Mwaya, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Mkokwa, vyumba 2 na ujenzi wa matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Njugilo kata ya Ipande, ujenzi wa vyumba 4 katika shule ya msingi Sama.
Pia kamati ya Ujenzi, Uchumi na mazingira wameweza kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa matundu 12 ya vyoo katika shule ya sekondari Kajunjumele, umaliziaji wa maabara katika shule ya sekondari Bujonde, ujenzi wa zahanati ya Isaki katika kata ya Katumbasongwe, ujenzi wa zahanati Kasumulu katika kata ya Ngana, ujenzi wa zahanati ya Ibungu katika kata ya Ikimba.
Kamati ya Fedha, uongozi na Mipango pia imeweza kutembelea miradi ya Kitalu cha michikichi kilichopo katika ofisi za Halmashauri, ujenzi wa matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi ndandalo, ujenzi wa shule mpya ya mchepuo wa kingereza inayojengwa katika kata ya Njisi, Mradi wa kusindika na kukoboa mpunga Kikusya katika kata ya Itope, ujenzi wa zahanati ya Mwambusye katika kata ya Ikama, mradi wa Trecka jipya litakalosaidia kuzoa taka ili mji wa Kyela uwe safi, kukagua mradi wa machinjio Ipinda na kutembelea boti mpya katika bandari ya kiwila, boti iliyonunuliwa na Halmashauri kwa ajili ya kuzuia uvuvu haramu.
Miradi hii yote inatekelezwa kwa nguvu ya pesa kutoka serikali kuu, pesa kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kyela, wadau mbalimbali pamoja na wananchi wanaochangia rasilimali fedha na nguvu kazi.
Aidha Waheshimiwa madiwani wameweza kutoa ushauri na maelekezo juu ya umaliziaji na utekelezaji wa miradi hiyo, Wameshauri kuanza kutumika kwa Trecka na Boti haraka ili kuwahudumia wananchi ambao ndio walipa kodi na wadau wakubwa wa maendeleo, utoaji wa taarifa ya mapato na matumizi katika mashine ya kusindika na kukoboa mpunga ya kikusya, ushauri uliotolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Katule G. Kingamkono.
Pamoja na hayo Mhe. Kefa Osca Mwang'anda diwani wa kata ya Ndandalo aliwashauri watalaam kufanya marekebisho katika miradi yote ambayo waheshimiwa wameshauri kurekebishwa.
Mwisho waheshimiwa Madiwani waliweza kutoa pongezi zao za dhati kwa wananchi wote, ambao wamekuwa ni mstari wa mbele katika kuchangia pesa na nguvu kazi na kuifanya wilaya ya Kyela kungara sana katika suala la utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kama ilani ya chama tawala inavyoeleza.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa