Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule Kingamkono amehamasisha shughuli ya upandaji wa miti wilayani Kyela, kazi iliyofanyika katika shule ya sekondari Kajunjumele, tarehe 16-04-2024.
Katika zoezi hilo Mhe. Katule amepata fursa ya kutoa elimu kwa wananchi na wanafunzi juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti katika mazingira yanayoizunguka jamii.
Mhe. Kingamkono amewataka wananchi kuwa na tabia ya upandaji wa miti katika kingo za mito ili kuondokana na maafa mbalimbali kama vile mafuriko na upepo katika miezi ya mvua.
Hata hivyo Mhe. Katule amesisitiza kuwepo kwa utaratibu maalumu ambapo pindi mti ukikatwa mara moja upandwe mwingine, kwa kufanya hivyo tutairudisha Kyela yetu katika hali ya ukijani na kupendeza.
Pamoja na hayo Mhe. Katule Kingamkono amesisitiza na kuwataka wananchi pamoja na wanafunzi katika kata ya Kajunjumele kulinda uoto wa asili lakini pia kuilinda milima yetu kwakuto kata miti hovyo kwa lengo la kupata maeneo ya kilimo kwani madhara yake ni makubwa kuliko faida.
Mwisho Mhe. Katule Kingamkono amewataka viongozi kuwa walinzi mazingira asili na kuwachukulia hatua watu watakao onekana wanafanya uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti kiholela, pia amechukua fursa hiyo kutoa pole kwa wananchi kwa maafa yaliyo ikumba shule ya sekondari Kajunjumele ikiwemo uharibifu wa miundombinu ya shule kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa