Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis (katikati) akiwa anapewa elimu kuhusiana na faida ya zao la kakao. Wapili kutoka kushoto ni mwenyeji wake Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis aipongeza halmashauri ya wilaya ya Kyela kwa miradi yenye tija.
Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwa katika eneo la bwawa la ufugaji wa samaki.
Mheshimiwa Naibu waziri ameyasema hayo leo tarehe 18/10/2023, alipofanya ziara ya kutembelea kitalu cha miche ya michiki cha halmashauri ya wilaya ya Kyela, bwawa la kufuga samaki, mtambo wa kutotoresha vifaranga vya samaki pamoja na eneo la shamba la mkulima al maarufu Mzee Tiptop anaepatikana katika kata ya Ibanda.
Akiwa katika eneo la uzalishaji wa miche ya miti ya chikichi, Mheshimiwa Khamis Hamza Khamis, amepongeza jitihada zinazofanywa na wataalamu wa halmashauri ya wilaya ya Kyela, kwa kupanda miche ya michikichi na kuigawa bure kwa wananchi.
Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwa katika eneo la mtambo wa kuzalishia vifaranga vya samaki katika ofisi za Idara ya kilimo wilayani Kyela.
Hata hivyo Mheshimiwa Naibu waziri ameitaka halmashauri ya wilaya ya Kyela kuongeza uzalishaji wa miche hiyo, ili kuongeza usambazaji wa miche hiyo kwa wananchi.
Aidha Mheshimiwa Naibu waziri amesifu mradi wa ufugaji na utitoreshaji wa vifaranga vya samaki na kuviuza kwa bei rahisi kwa wananchi kazi inayofanywa na halmashauri ya wilaya ya Kyela.
Pia amesema elimu ya ufugaji wa samaki izidi kutolewa kwa wananchi kwani kufanya hivyo, itasaidia wananchi kuachana na uvuvi haramu na kuanza shughuli za ufugaji wa samaki majumbani.
Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwa nyumbali kwa mkulima na mfugaji maarufu "mzee TipTop" kushoto, akipata elimu dhidi ya matumizi ya nishanti " Biogas" mbadala kwa matumizi ya kupikia.
Akiwa katika shamba la mzee tiptop mkulima maarufu wilayani Kyela, Mheshimiwa Khamis Hamza Khamis, amempongeza mkulima huyo, kwa kutumia nishati mbadala "biogas" na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae amekuwa akihamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kulinda mazingira.
Amewataka viongozi wa wilaya ya Kyela, kumtengenezea mazingira wezeshi Mkulima huyo ili aweze kupita na kutoa elimu kwa wanafunzi kwa shule zilizopo wilayani Kyela.
Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwa nyumbali kwa mkulima na mfugaji maarufu "mzee TipTop" kushoto, akipata elimu dhidi ya upandaji wa mti wenye uwezo wakuzaa tunda zaidi ya aina moja.
Pamoja na hayo Mheshimiwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira alipata fursa ya kupanda mti ikiwa ni ishara ya kuunga mkono jitihada za utunzaji wa mazingira, unaofanywa na wadau wa mazingira wilayani Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa