Halmashauri ya wilaya ya Kyela kwa kushirikiana na Ofisi ya Muhifadhi mazingira "TFS" tarehe 13/10/2023 wametembelea kata ya Ngana kijiji cha Ngana ili kutoa elimu ya kuwataka wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo katika mazingira ya vyanzo vya maji na ndani ya hifadhi ya misitu.
Mafunzo yaliongozwa na Mhifadhi misitu bwana Revocatus Frumence, akiwa ameongozana na Afisa mazingira bwana Godwin Gosbert, Eng. Venance Nkolabigawa pamoja na Salehe safi kutoka RUWASA.
Aidha elimu iliyotolewa ni pamoja na kuwasisitiza wananchi kuacha shughuli za;
Uchomaji wa mkaa, uvunaji haramu wa kuni na mbao, kilimo cha kuhamahama, malisho ya mifugo hususani kipindi cha masika katika vyanzo vya maji, uvuvi wa samaki kwenye skimu za umwagiliaji, uwindaji wa wanyamapori na kulima kwenye vyanzo vya maji au ndani ya mita 60.
Ndugu Revocatus amesema, kutokana na shughuli hizi za kibinadamu athari zifuatazo zimeonekana kwa jamii ya kata ya Ngana ikiwemo,
Kupungua maji ya mto Kandete na Mwega ambayo zamani ilikuwa inatiririsha maji mwaka mzima, kuhamia kwa nyani majumbani na kwenye michikichi baada ya kukosa chakula na hifadhi porini, uchache wa maji, kwenye skimu za umwagiliaji za mashamba ya mipunga, uhaba wa uzalishaji wa chakula pamoja na kupungua kwa maji katika chanzo cha mto Mwega-Ngana group.
"Hifadhi mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho"
Mwisho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa