Halmashauri ya wilaya ya Kyela imetoa mafunzo ya uboreshaji wa upimaji wa VVU na UKIMWI kwa wahudumu wa afya hapa wilayani Kyela . Mafunzo haya yametolewa katika ukumbi wa hospitali ya wilaya tarehe 12/11/2018.
Lengo kuu la kufanya mafunzo haya ni kukumbushana juu ya mambo yakuzingatia kabla ya kumpima mteja, umuhimu wa kuzingatia usafi, pamoja na njia za kumshawishi muathirika wa VVU/UKIMWI, ili aweze kuwaruhusu familia yake yote kupima na kutambua afya zao.
Aidha ndugu Notbulga Mmenuka amesema kwamba, wilaya ya Kyela imeanza ukamilishaji wa asilimia 90 ya kwanza kati ya asilimia 90 tatu, yaani hadi kufikia mwaka 2020 wilaya ya Kyela iwe imefikia malengo ya asilimia 90,90,90.
Nae muunguzi mwanafunzi Mary Lukasi wa zahati ya Ndwanga amesifia mafunzo yanayotolewa na amesema mafunzo haya wameyapokea vizuri na aliomba Halmashauri iendelee na kutoa elimu hii. Kwani lengo kubwa ni kuwasaidia wananchi kupata huduma bora kwa ujumla wake.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji,
Kitengo cha Habari na mawasiliano
Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa