Halmashauri ya wilaya ya Kyela kupitia Idara ya Afya kitengo cha lishe, imefanikiwa kutoa matone ya vitamini A kwa watoto 40,452 kati ya watoto 42,396 ambayo ni 95.4% katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022.
Taarifa hii imetolewa na Afisa lishe wa wilaya bi. Napendael Philemon alipokuwa akiwasilisha taarifa yake ya robo katika kikao cha kamati ya lishe kilichofanyika tarehe 15/10/2021.
Pamoja na hayo, Afisa lishe hiyo amesema Idara ya Afya kupitia kitengo cha lishe wamefanikiwa kutoa elimu ya chakula bora cha watoto, kufanya usimamizi shirikishi na elekezi wa huduma za Afya, pamoja na uhamasishaji wa kilimo cha bustani za mbogamboga mashuleni.
Mkurugenzi Mtendaji ambae ndiye Mwenyekiti wa kamati ya lishe, ndugu Ezekiel Magehema, akimkabidhi fedha mjumbe wa kamati ya lishe ndugu Omary Mbawala, ikiwa ni kumtia moyo kwa kazi anayoifanya ya kuhamasisha masuala ya lishe kwa kugawa mbegu za mboga mboga anazonunua kwa pesa yake, kwa ajiri ya kilimo cha bustani.
Aidha Mwenyekiti wa kikao hicho ndugu, Ezekiel H. Magehema amesema, kwa sasa suala la lishe latupasa kuliweka kama agenda ya kudumu katika vikao vyetu, kwani kwa hali tulionayo kila mmoja wetu ni mgonjwa. Uwe mnene au mwembamba kila mmoja na shida yake katika mwili, hivyo elimu ya vitamini A, ni lazima iendelee kutolewa kila mahali.
Pia aliwasisitiza wajumbe kuendelea kuchanja chanjo ya UVIKO 19, ili kujilinda na ugonjwa huu hatari wa corona
Katibu wa kamati ya lishe ndugu Mariam Ngwere akimkabidhi fedha mjumbe wa kamati ya lishe ndugu Omary Mbawala, ikiwa ni kumtia moyo kwa kazi anayoifanya ya kuhamasisha masuala ya lishe kwa kugawa mbegu za mboga mboga anazonunua kwa pesa yake, kwa ajiri ya kilimo cha bustani.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa