Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mheshimiwa Katule G. Kingamkono(shati la drafti) akikabidhi hundi ya mfano ya shilingi 150,000,000/= kwa vikundi 12 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika ukumbi wa Mamlaka ya Mji Mdogo Kyela.
Halmashauri ya wilaya ya Kyela imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi 150,000,000/= tarehe 16/11/2021 kwa lengo la kuwasaidia wananchi waliopo katika makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Akikabidhi mikopo Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Katule G. Kingamkono amesema, mikopo inatolewa kwa lengo la kuwasaidia wananchi kutoka tabaka la chini kwenda tabaka la juu, na mikopo hii inatokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Pia aliwataarifu wananchi kuwa Halmashauri inakusidia kutafuta kikundi cha mfano ili kukikopeshwa shilingi milioni 50,000,000/= kwa maendeleo yao.
Mwisho aliwaasa wanavikundi kuto vurugana mara tu yakupata mikopo yao kwani umoja na ushirikiano ndio nguzo ya mafanikio baina yao.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa