Akifungua mafunzo kwa wanavikundi 15 leo tarehe 03/05/2022, Mheshimiwa Katule Kingamkono Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, amesema,
Anapenda kutoa pongezi kwa Mhe. Rais kwa kuweka sheria ya kukopesha mikopo, kwani halmashauri ya wilaya ya Kyela inategemea kutoa mikopo yenye thamani ya shs milioni 150 kwa vikundi 15, Pia alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji ndugu Ezekiel Magehema kwa kusimamia makusanyo hadi kufanikiwa kutoa mkopo huu kwa vikundi, Hata hivyo, Mhe. Mwenyekiti aliwaomba wananchi ambao wanapata mikopo hii, wakawe mabalozi kwa wananchi wengine hasa kwa kutoa elimu ya kulipa ushuru.
Pia aliwataka kuwa walinzi kwa wote ambao wanatorosha mapato, kwani faida ya mapato ni haya ambayo leo wanayapata.
"Mkipata fedha hizi mkazifanyie malengo amabayo mmejiwekea, na niwaahidi miongoni mwa vikundi vilivyokopeshwa mwaka huu, kikundi kitakachorejesha vizuri watakopeshwa shs milioni 50".
Mwisho aliwaomba wananchi kuwaombea viongozi hasa waheshimiwa madiwani kuongoza vizuri, ili waendelee kuwa na moyo wa kupitisha mikopo hii.
Nae Afisa Maendeleo ya jamii, amesema, wao wanafanya mchakato wa kuzidi kutafuta kikundi ambacho kitafanya vizuri ili kiweze kupewa mkopo huo wa shilingi milioni 50.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanavikundi, ndugu chaula (mwanakikundi)amesema, anaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutuona wananchi, pia aliahidi kwa niaba ya wenzake kuwa, pesa hizi wanazozipata wata watakwenda kuzitumia kadili walivyojipangia.
Halmashauri ya wilaya ya Kyela hadi sasa imeshatoa zaidi ya shilingi milioni 490, ikiwa ni mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa