Haya yamezungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, Mhe.Lucy L. Mganga, alipokuwa akifungua semina elekezi ya usimamizi wa mitihani ya darasa la nne, iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, tarehe 12/11/2018.
Aidha amesema, hatakuwa tayari kumvumilia msimamizi yeyote yule ambaye atasababisha matatizo katika zoezi hilo la mitihani, iwe ni kwa makusudi au kwa uzembe.
Pia aliwataka kuwa huru kusema, kama yupo msimamizi yeyote alie lazimishwa au hataki kuifanya kazi hiyo ajitokeze mapema kabla ya kuanza kazi hiyo.
Mitihani ya darasa la nne itaanza rasmi tarehe 22/11/2018 hadi tarehe 23/11/2018, hivyo kuwataka wasimamizi wote kutofanya kazi hiyo kwa mazoea.
Mwisho aliwatakia usimamizi mwema wa mitihani na kufungua rasmi semina hiyo.
Imetolewa na :
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa