Haya yamezungumzwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Claudia U.kitta alipokuwa akiongea na vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, katika hafla fupi ya kukabidhi mfano wa hundi ya mikopo yenye thamani ya shilingi 140,000,000/= .
Hafla hii imeandaliwa na Idara ya maendeleo ya jamii iliyofanyika katika ukumbi mkubwa wa halmashauri ya wilaya ya Kyela tarehe 16/12/2020.
Akizungumza kabla ya kukabidhi Hundi hiyo Mhe.Mkuu wa wilaya amesema, Hii ndio serikali inayongozwa na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Na serikali hii inatimiza maagizo yote yaliyopo katika ilani ya chama. Hata utoaji wa mikopo hii kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wanye ulemavu ni sehemu mojawapo ya utekelezaji wa ilani ya chama chetu.
Aidha Mkuu wa wilaya amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu Ezekiel H.Magehema kwa uwezo wake mkubwa wa kukusanya mapato ya serikali hadi kasababisha mikopo hii kutolewa kwa wakati.
Pia Mhe.Claudia U. Kitta amewataka wanavikundi kuwa na umoja ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea. Sababu pesa hizi ni kodi kutoka kwa wananchi, hivyo pesa hizi ni zao na wanapaswa kurejesha kwa muda ili kuwasaidia wananchi wengine.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela amesema, Kyela ni wilaya ambayo watu wake wakiamua kubadilika wataleta maendeleo makubwa katika wilaya. Kwani Kyela ni wilaya yenye fulsa nyingi ukilinganisha na maeneo mengine.
Hivyo aliwataka wanavikundi kutumia mikopo hii katika fulsa zilizopo Kyela, mfano upatikanaji wa michikichi, kokoa, mpunga na vitu vingine vingi. Pia aliwaasa wanavikundi kujiunga na mfuko wa iCHF ili wanapopata matatizo ya afya mfuko huo wa bima ya afya uwasaidie na si kutumia hela ya mkopo kwa matibabu.
Akizungumza kwa niaba ya wanavikundi Bi.Rehema Kalisa alitoa pongezi kwa viongozi wa wilaya kwa kuwawezesha wananchi kupata mikopo yao kwa wakati, aliwawaahidi viongozi hao kwenda kutumia mikopo hiyo kwa maendeleo ya jamii nzima.
Halmashauri ya wilaya ya Kyela imetoa mikopo kwa vikundi 27 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu, mikopo wenye thamani ya shilingi 140,000000/=.
Baadhi ya wanavikundi wakionesha bidhaa zao kwa viongozi bidhaa ambazo zimeyokana na mikopo kutoka serikalini.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa