Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela limekuwa ni miongoni mwa Mabaraza machache katika nchi ya Tanzania katika suala la matumizi ya TEHAMA, kwa kuanza kutumia vishikwambi katika vikao vyote vya kisheria.
Mwenyekiti wa Halamashauri ya wilaya ya Kyela Mheshimiwa Katule G. Kingamkono amesema, Baraza la madiwani wilayani Kyela limeamua kuanza kutumia teknolojia kwa sababu ya kupunguza gharama za uandaaji wa vikao hivyo, hasa katika suala la ununuzi wa shajala za maandalizi ya vikao hivyo na kupunguza gharama za mafuta ya kusambazia makabrasha ya vikao hivyo vya kisheria. Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya matumizi ya vishikwambi hivyo kwa Waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kyela leo tarehe 28/10/2022.
Hongereni viongozi wetu kwa kutambua matumizi ya TEHAMA na kupunguza gharama kwa serikali hasa katika suala la maandalizi ya vikao ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya muda kwa matumizi ya teknolojia hiyo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa