Akihitimisha zoezi la ufungaji wa mafunzo kwa vikundi na utoaji wa hundi ya mfano kwa vikundi 15, Leo tarehe 6/06/2022 Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Ismail Mlawa amesema,
Serikali imekuwa na dhamira njema kwa wananchi wake, serikali inakopesha pesa kwa wananchi,Na ikiwa pesa hizi zitasimamiwa vizuri na zikarejeshwa basi wananchi wengine watafaidika. Amesema si serikali zote zinafanya hivi, bali ni serikali ya Tanzania.
Aidha amesema pesa hizi hazina riba, lengo ni kutaka kuleta tija kwamba serikali yetu inalengo mahususi la kuwaondolea wananchi wake umaskini.
"Ni imani yangu kwamba mmepewa elimu ya kutosha na mtakwenda kuzitumia pesa hizi kadili mlivyopanga" alisema Mhe. Mkuu wa wilaya.
Pamoja na hayo Mheshimiwa Mkuu wa wilaya amesema, wapo watu wengi wamefaidika na mikopo hii, hivyo endapo tutaitumia vizuri basi wote tutafaidika.
Pia aliwasa viongozi wa vikundi kwenda na kusimamia vikundi vyao, hasa katika fedha walizozipata, ili ziwatoe hatua moja kwenda hatua nyingine.
Vikundi 15 vimefaidika na mkopo kwa robo hii ya Mwaka huu wa fedha.
Aidha kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Kenneth Nzilano amesema, Halmashauri yetu ilijipanga muda mrefu, katika suala la utoaji wa mikopo ndio maana tumefanikisha kutoa mikopo kama tulivyopanga.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wanavikundi wenzake, ndugu Atupikile Mwabwagilo
Amesema, anaishukuru sana serikali kwa kuwaona wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kwani tumepewa mafunzo pia tumepewa na mikopo, aliahidi kwa kusema mkopo waliopewa wataurejesha kama ilivyopangwa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa