Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Josephene Manase amekabidhi mfano wa hundi ya mkopo wa 10% Tsh. 816,831,820.00 iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya Wanawake,Vijana na watu wenye Ulemavu katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 11.2.2024.
Akikabidhi hundi hiyo Mhe. Mkuu wa Wilaya ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwakumbuka wananchi wake kwa kutoa mkopo huo.
Mhe.Mkuu wa Wilaya amewapongeza wanufaika wa mkopo huo na kuwasihi kutumia vizuri fedha watakazopata ili waweze kujikwamua kiuchumi,kufanya shughuli za maendeleo ili waweze kufikisha malengo yao.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewaasa wanufaika hao kurejesha mkopo kwa wakati ili watu wengine waweze kunufaika,pia amewataka Wanufaika kuwa mabalozi wazuri katika maeneo yao juu ya suala upatikanaji wa mkopo.
Pia Mhe.Manase amewaonya wale wote wanaotumia kigezo cha mkopo kutapeli watu, kuacha mara moja tabia hiyo kwani wakibainika hatua kali za kisheria zitachukiliwa dhidi yao.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Bi.Florah A. Luhala ameipongeza Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kufanya mchakato mzima tangu usajili wa vikundi na ufuatiliaji wa fedha hizo ili kuhakikisha zinawafikia walengwa.
Sambamba na hilo,Bi.Flora A.Luhala amesema mkopo huo ukawe chachu ya kubadilisha maisha kwa kufanya shughuli za maendeleo zitakazowasaidia kujikwamua kiuchumi.
Wakizungumza kwa niaba baadhi ya wanufaika wa mkopo huo wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea mkopo huo kwani utawasaidia kujiondoa kwenye mkopo wa kausha damu ambao umekua changamoto miongoni mwa wananchi wengi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa