Mkuu wa Idara ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe amemkabidhi ndugu Stephen Mwakitema vifaa mwendo kwa niaba ya watumishi wa afya na wadau mbalimbali waliochangia ununuzi wa vifaa hivyo.
Ndugu Stephen amekabidhiwa vifaa hivyo mara baada ya kupata changamoto ya kiafya iliyompelekea kukosa uwezo wa kutembea bila msaada.
Aidha viti mwendo vilivyokabidhiwa ni kwa ajili ya kumsaidia kumsogeza akiwa ndani na kingine kitakachoweza kumfikisha maeneo mbalimbali ya kijamii hivyo kumfanya aweze kujumuika na jamii katika masuala mbalimbali.
Aidha ndugu Stephen ameishukuru sana Idara ya afya na Halmashauri kwa ujumla kwa jinsi ambavyo wamemthamini kwa hali ya afya aliyokuwanayo kwa sasa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa