
Mkuu wa idara ya afya ustawi wa jamii na lishe Dr. Saumu S. Kumbisaga akiwa katika kikao kazi cha wafawidhi na CHMTs katika kuhakikisha huduma za Afya katika Wilaya ya Kyela, zinaboreshwa na kupunguza kero kwa wananchi
Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa idara ya Afya tarehe 18/07/2024.
Katika kikao hicho tathmini ya utendaji kazi ilifanyika, katika idara ya Afya na kuweka mikakati madhubuti kuondoa kabisa changamoto zote zilizojitokeza kwa mwaka wa fedha 2023/2024, ili kuanza mwaka mpya wa fedha 2024/2025 kwa ari na nguvu mpya.
Aidha katika kikao hicho, Mkuu wa idara alisisitiza uadilifu kazini, ushiriki wa wafawidhi katika mikutano ya vijiji na kata, ili kutoa elimu ya afya kwa jamii inayowazunguuka hasa katika afya ya uzazi na mtoto, magonjwa ya milipuko,
Pia amesisitiza kuhakikisha jamii inatumia huduma za afya zilizo karibu yao, kwani Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amehakikisha amesogeza huduma za afya kwa jamii pia ameboresha miundo mbinu na kuendelea kuleta watumishi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa