Hayo yameingizwa na katibu tawala wa halmashauri ya wilaya ya kyela mhe. Kawacha alipotembelea miradi ya mwenge wa uhuru iliyopo wilayani kyela katika kata ya mababu na kata ya matema tarehe 30/07/2019.
Katibu tawala wa halmashauri ya wilaya ya kyela alitembelea jumla ya miradi 6 itakayopitiwa na mbio za mwenge wa uhuru tarehe 06/09/2019 yote ikiwa na thamani ya shilingi milioni 459, 143, 508.4 ambayo yote hii imetokana na utekelezaji wa serikali kuu kupitia halmashauri ikishirikiana na wadhamini wakiwemo Bioland.
Aidha ametoa pongezi kwa wadau wote walioshiriki katika utekelezaji wa miradi hiyo na kuwataka viongozi waendelee kusimamia vyema miradi hiyo mpaka ifikapo tarehe 25/08/2019 iwetayari kupisha uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru utakaofika wilayani kyela mnamo tarehe 06/09/2019.
Mwenge wa uhuru unatarajia kuingia wilayani kyela mnamo tarehe 06/09/2019 ukiwa ni mwendelezo wa uzinduzi wa miradi ya maendeleo kwa mwaka huu wa fedha 2019/2020 kupitia kauli mbiu yake ya “ Maji ni haki ya kila mtu tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa”.
Hata hivyo serikali yetu ya awamu ya tano ya Dkt. John Magufuli imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha huduma zote za kijamii zinaboreshwa ikiwemo huduma ya maji, Afya, miundombinu, pamoja na elimu lengo likiwa ni kuhakikisha kila mtu anapata huduma mhimu bila kujali hali yake ya kiuchumi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa