Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji mdogo wa Kyela Mhe. Josephat Longoli alipokuwa akitoa hotuba yake, katika kikao cha Baraza kilichofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya mji mdogo Kyela tarehe 18/09/2018.
Akizungumza na wajumbe wa kamati tendaji za kudumu za Mamlaka ya mji mdogo wa Kyela, Mhe. Josephat Longoli amesema, Mamlaka ya mji mdogo imefanya mkataba na jeshi la magereza Kyela, ili kuwatumia wafungwa katika kufanya usafi katika mji wa Kyela.
Usafi utakaofanywa na jeshi hilo ni pamoja na kusafisha mazingira yote ya mji wa Kyela, pamoja na kuzibua mitaro yote ya maji iliyoziba ikiwa ni pamoja na kuisafisha mitaro hiyo.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji mdogo wa Kyela, ameongeza kwa kusema Mamlaka imenunua eneo la maziko kwa mtu yeyote atakaefikwa na umauti, eneo hilo ni eneo linalopatikana katika Kata ya Itope, badala ya kuendelea kutumia eneo la bondeni ambalo kwa sasa eneo hilo limejaa.
Aidha shilingi 22600000/= zilitengwa katika mwaka wa fedha wa 2017/2018, na fedha hizo zimetumika katika shughuli za maendeleo kama ujenzi na ukarabati wa shule mbalimbali, ikiwemo shule ya msingi Nyasa English medium, shule ya msingi Kyela kati, na ujenzi wa makalavati katika maeneo sumbufu.
hata hivyo katika bajeti ya 2018/2019, Mamlaka imetenga fedha kwa ajiri ya kununua gari la kuzolea taka, Mamlaka inafanya haya kwa ajiri ya kuunga mkono kwa Serikali ya awamu ya tano ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka mazingira safi.
Mwisho aliwatoa hofu wajumbe wa kikao ambao walihoji juu ya bakaa ya fedha, alisema Mamlaka inategemea kupata majibu ya bakaa ya fedha yao kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kyela ndani ya mwezi huu, na majibu hayo yataletwa kwa wajumbe wakikao hicho.
Imetolewa na :
Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya
Ofisi ya Habari na Mawasiliano
Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa