Waheshimiwa Madiwani 9 wakiongozana na maafisa 2, mwandishi wa habari 1, kutoka wilayani M’mbelwa mkoani Mzimba nchini Malawi, wamefanya ziara hapa nchini katika wilaya ya Kyela wakiwa na lengo la kujifunza shughuli zinazofanywa na kamati ya fedha ya waheshimiwa madiwani, mikakati inayofanywa na wilaya katika kukusanya mapato, shughuli zinazofanywa na baraza la madiwani, kazi zinazofanywa na waheshimiwa madiwani katika kuleta maendeleo ya nchi, Mahusiano baina ya Baraza la madiwani na ofisi ya Mkuu wa wilaya, pamoja na idara mbalimbali zinavyotoa huduma kwa wananchi.
Ziara hiyo imefanyika tarehe 02/06/2021, ambapo wageni hao walipokelewa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Mheshimiwa Katule G. Kingamkono katika eneo la Boda Njisi na kisha kuwapeleka hadi katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kyela.
Akiongea na Mkuu wa wilaya ya Kyela, Kaimu Mkuu wa wilaya ya M’mbelwa Nchini Malawi Mheshimiwa Steve Chima amesema, wameamua kufanya ziara katika Nchi ya Tanzania katika wilaya ya Kyela kwa lengo kubwa la kutambua ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili, ikiwa ni pamoja na kujifunza njia zinazotumika katika kukusanya mapato ya serikali.
Nae Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Claudia U. Ktta aliwapongeza wageni hao kwa kuona fahari kutembelea nchi yetu hususani katika wilaya ya Kyela. Alisema ziara hii, inaongeza mahusiano mazuri zaidi baina ya nchi zetu.
Aidha waheshimiwa madiwani kutoka nchi ya Malawi walipata fulsa ya kufanya kikao kifupi na waheshimiwa madiwani kamati ya Fedha wa Tanzania katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kyela. Wakiendelea na kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, ndugu Ezekiel Magehema kwa kupitia afisa utumishi wa wilaya, aliweza kutoa taarifa fupi ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na wataalam wakishirikiana na Waheshimiwa madiwani , ambapo taarifa hiyo iliibua majadara mzuri baina ya Waheshimiwa madiwani kutoka nchi ya Malawi na waheshimiwa madiwani wa hapa nchini Tanzania. Katika mjadara huo waheshimiwa madiwani kutoka Nchi ya Malawi waliweza kufahamu jinsi kikosi kazi cha ukusanyaji wa mapato(Task Force) kinaweza kufanya kazi ya ukusanyaji wa mapato bila kuathiri au kudhurumu haki za wananchi.
Mwisho Mwenyekiti wa Baraza la madiwani Nchini Malawi Mhe.Wishart A. Malinga alitoa pongezi za dhati kwa ukarimu wa WaTanzania na aliwaomba Waheshimiwa madiwani wa wilaya ya Kyela kufanya ziara nchini Malawi ili nao wapate kujifunza mambo mbalimbali ya maendeleo katika nchi hiyo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa